*UFUMBUZI WA AINA 3 ZA UZALIWA WA KWANZA*
🌲 _Katika maisha kuna vitu unatakiwa kutafakari unapo viona, au kuvifanya, vijana hii imekuwa changamoto kwao kuishi maisha yasiyo na hofu ya Mungu, huku ni kutengeneza maisha magumu ya baadaye_ Katila Somo hili la *, _Uzaliwa wa Kwanza wa Mwili Wako Umemuuzia Nani_* kuna changamoto ya watu wanaopoteza uzaliwa wa kwanza wa miili yao ni wale wanaoijua kweli tayari, hii ndo laana kubwa kwa ndoa za watu wengi. *Waebrania 10:26-29*
26 *_Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi;_*
27 bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao.
28 Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu.
29 _Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?_
🌲Kweli Mungu ni wa rehema, anasamehe pale tunapo tubu, laini huwezi kuwa kama mtu aliye jilinda na kushinda zinaa akaingua katika ndoa akiwa mwaminifu juu ya mwili wake.
🌲 _Kuna watu wanasema, na wale ambao wamepoteza uzaliwa wao wa kwanza wa miili yao(Ubikra) kabla ya kuokoka itakuwaje sasa, _Jibu ni jepesi, katika ujinga wao na upofu wao walipoteza uzaliwa wa kwanza wa miili yao, hairudi Tena lakini wakimjua Mungu waliye mpokea baada ya kuokoka na wakawa waaminifu nakichukia dhambi, na uovu waloutenda, wakaandamana na Yesu kwa bidii, hupewa neema ya Heshima ya Uzaliwa wa Kwanza wa Wokovu iliyo kuu Kufunika mapungufu ya uzaliwa wa kwanza wa mwili ulopotezwa, na hiyo huwafanya waishi kwa furaha na Amani._
🌲Ila duniani ulifanya vibaya, ukapoteza uzaliwa wa kwanza wa mwili wako, umekuja kwenye wokovu, umeendeleza tabia ya zinaa, leo umetubu, kesho umeanguka kwenye zinaa, kwa mtu huyu anagharama kubwa ya kulipa katika maisha yake.
🌲_Msisitizo hapa, ukiokoka acha zinaa, hakuna lugha za nimejaribiwa, nimelemewa na hisia, bahati mbaya, huna utetezi, mazingira yako yatazidi ya Yusufu? *Waebrania 12:1*
*_Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu,_*
🙏�🙏 _�Ninapo hitimisha Somo hili ni watie moyo vijana, na kuwatamanisha vitu vya baraka, aisee ukiingia kwenye ndoa ukiwa mwaminifu, na Uzaliwa wako wa kwanza wa mwili(Ubikra) uwe kijana wa kike au wa kiume, kuna mambo yafuatayo unaya feel (unaya hisi)_
👉� *Unahisi Kupendwa sana, na kumpenda sana mwenzako*
👉� *Unahisi Kumwamini, na kuaminiwa sana na mwenzako*
👉� *Unahisi kuwa huru na kufanya mambo yako yote ya kifamilia na ya kiroho kwa uhuru na amani*
👉� *Unajiona shujaa, hodari na jasiri unayeweza elekeza wengine kwa ushahidi wa ushindi si kwakutumia makosa yako, (hiyo inaumiza)*
👉� *Unaishi bila Psychological Questions, (If, May be, I regret, No way out etc) haya ni maswali ya hatari katiks ndoa. Kila aliyetumbukia kwenye zinaa na hasa baada ya kuokoka maswali haya yamewatesa kwenye ndoa*
❤❤ _Ebu fanya maamuzi yakutopoteza uzaliwa wa kwanza wa mwili wako, na kama umeisha poteza rudi kwa Yesu kwa toba ya dhati, na uwe mwaminifu kweli_❤❤
*_Ev. Elisha Kazimoto_*
*0755444078*
No comments:
Post a Comment