💞💞 *K̥ͦW̥ͦḀͦ N̥ͦI̥ͦN̥ͦI̥ͦ K̥ͦU̥ͦC̥ͦH̥ͦO̥ͦK̥ͦḀͦN̥ͦḀͦ K̥ͦḀͦT̥ͦI̥ͦK̥ͦḀͦ N̥ͦD̥ͦO̥ͦ*💞💞
*_B̥ͦy̥ͦ E̥ͦv̥ͦ.E̥ͦl̥ͦi̥ͦs̥ͦh̥ͦḁͦ K̥ͦḁͦz̥ͦi̥ͦm̥ͦo̥ͦt̥ͦoͦ(B̥̥ͦͦḁͦb̥ͦḁͦ E̥ͦv̥ͦe̥ͦ)_*
*0755444078*
_Shalom wana ndoa,mlooana kwa kusudi la Mungu,kwa upendo mkuu,na gharama kubwa ya kulipa Maali na kufanya sherehe kubwa na Kuwathibitishia watu wote kanisani kwa *Kiapo cha Ujasiri kabisa*Kuwa nitakupenda,nitakulinda,na kuwa na wewe sikuzote za maisha yangu,nitawaacha wanawake/wanaume woote,nakuambatana na wewe siku zote,na kumalizia na neno zuuri, *"Ee Mungu Nisaidie"*,sasa kuchokana huko kumetoka wapi?_
✍Basi mtaalamu na Mwana Saikolojia,mchambuzi wa masuala ya Mahusiano na Ndoa, *Ev.Elisha Kazimoto(Baba Eve)* nitakujuza yakupasayo kuyaangalia ili urejeshe ndoa yako katika siku ya kwanza ya Kiapo cha Upendo.
✍ _Wana ndoa,kabla ya kuangalia,kwa nini tunachokana,Julize ilikuwaje,kulikuwa kuna nini tunafanya,pale mwanzo mpaka tukawa tunapendana sana,shahuku ya mwenzako asikae mbali nawe ilikuwepo,kipindi hicho,tulikuwa tunafanya nini?_
✍ kumbuka Biblia haisemi *Ukatubu* inasema, *_Kumbuka ni wapi ulipo anguka Ukatubu_* kuna umuhimu wa kufanya marejeo ya upendo wenu wa awali ulikuwa unasukumwa na nini hata kuwa mkubwaa?hapo ndo mnaweza anza harakati za kutibu ndoa yenu unapo hisi kumchoka mwenzako.
*_Ufunuo wa Yohana 2 : 5 - Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu._*
✍wana ndoa,kabla ya mambo yote,kumlaumu mmeo,mkeo au chochote,Kumbuka niwapi ulipo poteza matendo ya kwanza katika ndoa yenu,yaliyo kuwa yanakufanya hata akiondoka siku moja,unahisi ni mwaka,akicheka unatamani asiache,akizungumza unatamani uendelee kusikia maneno yake,kumbuka yale matendo umeyapotezea wapi? *_Ulipo pata pesa?,Ulipo pata mtoto?ulipo pata kazi?Ulipo anza kusema uongo?ulipo anza urafiki na mashosti wako?Ulipo anza kuwasikiliza ndugu zako na wazazi wako kuliko mkeo/mmeo? Kumbuka ukatubu(yaani. utengeneze)ukayatende yalee ya kwanza_* Huo ndo uponyaji wa Kuchokana.
✍ _Leo sitakuletea makara ndefu,fupi na tiba_ Mara hoo,mwenzangu siku hizi simuelewi! Kwa nini mwanzo mnachumbiana mpaka mnaoana,ulimwelewa? kwa nini saizi?kumbuka nini kilikuwa kinakufanya unamwelewa, *Kifanye hicho hicho ataeleweka tu*
✍ Mwanzoni ulikuwa unamwambia wewe ni mzuri,saizi umeacha,kwa nini msichokane?
✍Mwanzoni,ulikuwa unafua nguo,unamnyoshea,maji ya moto ya kuoga,andaa kila kitu mapema cha kula,leo anajiandalia,au ni house girl anaanda,kwa nini msichokane?
✍Mwanzoni tendo la ndoa,ilikuwa tu mnatumia ishara ya macho,umeisha jua kwamba hapa ni nusu fainali,saizi mpaka udanganywe,uahidiwe zawadi hewa,au ukabwe ndo unakubali,kwa nini msichokane?
*_Mwisho,wana ndoa rudisheni Matendo ya kwanza,ya uchumba na honeymoon na miezi 6 ya kwanza ya ndoa yenu,yawe ndo matendo yenu ya kila siku hamtachokana_*
*_By Ev.Elisha Kazimoto(Baba Eve)_*
*0755444078*
No comments:
Post a Comment