Monday, 9 January 2017

KWELI KUHUSU TENDO LA NDOA

*KWELI KUHUSU TENDO LA NDOA*
" *SWALI* _Hivi ni halali kwa wana ndoa kunyonyana sehemu za siri(Uume au Uke),Imekaaje Kiroho?_"
( *Mjibu swali:Ev Elisha*)
✍ Kwanza kabisa nikupongeze muuliza swali kwa ujasiri wa kutaka kuweka mambo sawa katika maisha ya ndoa,ili uweze kuwa na mahusiano mazuri na Mungu wako.
✍ _Nianze kwa kusema Tendo la ndoa ni pana sana,lakini kama jina lake lilivyo tendo la ndoa ni kwa wana ndoa tu,siyo kwa vijana wasio kwenye ndoa( Huo ni Uasherati-dhambi kubwa)au siyo nje ya mke/mme wako huo ni Uzinzi-dhambi na laana kubwa_ kwa hiyo *Sex* ni tendo halali kwa wana ndoa.
✍Ukilizungumza tendo la ndoa siyo tendo la kukutanisha viungo vya uzazi tu(in- and out) tu,bali ni pamoja na maandalizi ya michezo ya kimahaba( *Sex Plays*) zikiwemo romance(busu zito/denda),kutomasana,na michezo mingi ya kuibua hisia,kuamsha mwili ili uwe tayari kwa tendo la viungo kukutana kwa uzuri,wepesi,na kuleta raha kwa washiriki( _Ndiyo maana vijana ambao hamjaoa wala kuolewa ni marufuku kufanya michezo hii inayoibua hisia za kufanya ngono,lengo la michezo hiyo siyo kwasababu ni rafiki,au ni upendo mkuu kwa mwenzako,ni kuuamsha mwili wake uwe tayari na mwepesi kwa ngono,kwa hiyo mkiicheza hata msipo kutanisha viungo vya uzazi uume na uke,tayari mmezini,mmesheratika kwa mawazo,na Mungu ahukumu matendo tu ila mawazo yazaayo matendo mabaya_)
✍Sasa, *Kunyonyana viungo vya Uzazi(uume na Uke ni Sahiii kwa wana ndoa?*
Mtazamo wangu ni huu, Lazima kwanza tujue aina za tendo la ndoa(ngono) Types of Sex.
1. *Genital sex*( ngono ya kutumia viungo vya uzazi uke na uume kuingiliana )Halali kwa Mungu,ndiye aliye umba na akatoa kazi yake *Zaeni* Mwanzo 1:26-28, kwa aina hii haina maswali ni moja kwa moja inajulikana.(Japo tendo la ndoa si kwaajili ya kuzaa tu,ni pamoja na kustareheshana wana ndoa,na kutuliza mawazo)
2.  *Anal sex*(ngono ya Aja Kubwa)mwanaume kumwingilia kimwili mwanamke au mwanaume kwa nyuma,(kinyume na maumbile)( *Ulauwiti au Ufilaji*) Hii ni dhambi kubwa,laaana,imaleta ghababu ya Mungu haraka sana(matendo ya sodoma na gomora)
*_1 Wakorintho 6 : 9 - Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti._*
Kwa hiyo iwe kwa wana ndoa hamuruhusiwi,tumieni maumbile yenu,wengine huvunja mipaka ya Mungu kisa ni wana ndoa,wanafanya ngono hata ya nyuma kinyume na maumbile(Haja kubwa haikuumbiwa kuzalisha raha ya tendo la ndoa,unakosea sana).
3. *Oral Sex*(ngono ya mdomo) kama ilivyo ngono ya haja kubwa ndo ilivyo ngono hii,ila hii yaweza kuwa mwanaume au mwanamke,kutumia mdomo wake kunyonya na kumtosheleza mwenzi wake kingono. (hii nayo siyo Sahiii japo watu hupinga kwa kusema mbona kunyonyana ndimi(romance,siyo vibaya?iweke kunyonya nyeti ndo vibaya?)hoja nzuri( *Ni vizuri tujue kunyonyana ndimi ni mdomo kwa mdomo,viungo vinavyo fanana,vinavyo fanya kazi sawa vimetumika,siyo kimyime na maumbile*) tunge shangaa kama tungeona mtu ana nyonya kulamba haja kubwa tungesema ni kinyume na maumbile.
✍ _Mwana ndoa usibadili matumizi ya asili Mungu atawaacha......_
*WARUMI 1:21-28*
21 kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza. 

22 Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika; 

23 wakaubadili utukufu wa Mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu, na ya ndege, na ya wanyama, na ya vitambaavyo. 

24 Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao. 

25 Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina. 

26 Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili; 

27 wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao. 

28 Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa. 
✍Cheza michezo yote lakini zingatia matumizi ya asili ya  viungo vyenu
✍ *_Isitoshe mambo haya,yamekuja ikiwa ni maendeleo ya sayansi na technolojia,utandawazi ambapo wafanya ngono za biashara,wafanyao uchafu na machukizo,hufanya ngono,na kuona haitoshi shetani akaongeza mbinu chafu ikiwa imepakwa rangi ya utundu wa kitandani,kuwafanya watu wazidi kumchukiza Mungu hata wana ndoa,waingilane kinyume cha maumbile,nyuma na ndomoni,ikaongezwa nyingine ili kuzidi kuvuta ghadhabu ya Mungu,ikalewa ya usagaji,ushoga nk...tusipo kuwa makini tutakuta vyote tunaviona halali....lakini hayo yote ni matokeo ya Video za Ngono zinazo zidi kuja na navumbuzi mengi yaliyo jaa machukizo kwa Mungu_*
   _Ni hitimishe kwa kusema,Ni udanganyifu mkubwa wa shetani,kuona kuwa unaweza kumtosheleza mwenzako au kumfanya anogewe na mahaba kwa kushiriki naye ngono ya mdomo(Kunyonyana Nyeti zenu)_
   *_Unaonaje,Mungu akisitisha uwezo wa kuingiliana kwa viungo vyenu,uume na uke,mkabakiza kunyonyana nyeti zenu...Lengo na furaha ta ndoa na tendo la ndoa itafikiwa?_
      *Tafakari Chukua Hatua*
     _Mchambuzi Ev.Elisha Kazimoto(Baba Eve)_
     *0755444078*

No comments:

Post a Comment