💈💈 *USINGE DHARAU MAMBO HAYA MADOGO, NDOA YAKO INGEKUWA SALAMA*💈 💈
*_By Ev Elisha Kazimoto(Baba Eve)_*
(Psychologist & Counselor)
*0755444078*
💈 _Shalom, shalom mwana ndoa na mwana ndoa mtarajiwa, leo nakuja na uponyaji wa Mahusiano, Uchumba na Ndoa kwa pamoja ili tupunguze msongo wa mawazo au tuondoe kabisa hizo( *Stress*)za ndoa tuishi kwa furaha na huyo mke wa ujana wako_👇�👇�👇�👇
*_Mithali 5 : 18 - Chemchemi yako ibarikiwe; Nawe umfurahie mke wa ujana wako._*
💈Huwezi kumfurahia mke wako, mme wako kama mmeyasahau mambo madogo madogo ya kisaikolojia yanayo funika hisia, yanayo jaza kikombe cha upendo cha moyo, yanayo punguza na kufunika udhaifu wa mwenzako na kumuona mtu wa maana na kamili maishani mwako.
💈Ndoa ahiitaji misuli 💪, inahitaji akili sana, na maarifa, hapo utaifurahia ndoa yako. ( _Unaye jiandaa kuingia katika ndoa usijiandae kupambana, kukabiliana na mtu, jiandae Kisaikolojia kumpendeza mwenzako, kumlinda mwenzako, kumuhudumia mwenzako, kumtia moyo mwenzako, kumwambia wewe ni wapekee kati ya wanawake wote/wanaume wote wewe umewapita wote)_👇�👇�👇�👇
*_Mithali 31 : 29 - Binti za watu wengi wamefanya mema, Lakini wewe umewapita wote._*
💈Sijui kama unaelewa lugha hii na maana hii, yaani mpaka unamuoa huyo, au unakubali kuolewa na huyo, maana yake huyo ndo amewapita wote! _kama ulioana na huyo basi kwakuwa alikupa mimba polee(unahitaji msaada wa wana saikolojia tukusaidie umpende tu), kama ulioana na huyo kwakuwa wazazi walikutafutia, alikusaidia tu kulipa ada ya chuo, unahitaji msaada wa Kisaikolojia upende tu_
💈Sasa kama amewapita wote, *Mchepuko wa nini?* maana tendo la kumuoa, kukubali kuolewa naye si kwamba hawakuwepo wengine, ila uliona huyo ndo mtatembea pamoja, sasa kama ni hivyo ( *Mke wa pili wa nini?*)
_Kuna vitu unavikosea katika kuishi na mwenzako_
💈Leo Mtaalamu wa Mahusiano na Ndoa, *_Ev. Elisha Kazimoto_*na kualika ukae wq kujifunza ili ijue, mambo madogo, madogo ya kisaikolojia ulo yadharau ndo yamefanya *_Umchoke Mwenzio_* wakati kwanza, ndo mna watoto 2,miaka 5 ya ndoa, je mkisha kudlfikisha miaka 50 mtakuwa mnatafutana kwa panga🗡🔪🔫kuuwana? Ni wakati wa kubadiri MTAZAMO ndoa siyo vita wala nguvu ndoa ni Akili, na mimi leo Mwana Saikolojia nakupa Akili ya mambo madogo ulo ya sahau, yarudie, usiwe na aibu, huyo siyo mgeni ni mpenzi wako, yafanye usimwonee aibu kwamba atanishangaa nitaanza anzaje,? *_Anza hivyo hivyo kama ulivyo kiwa unaanza kumshushua mistari ya kumchumbia, au kumkubalia ombi lake, kwani ilikuwa rahisi? Ila si ulitimiza hazima yako? Si ndo maana mpo wote_*
💈Sasa Tuangalie haya mambo madogo yanayo hitaji akili ya kuzaliwa na ya mazingira siyo chuo wala sekondari yalivyo na nguvu kwa ndoa yako. _Tutanguliwe na Andiko hili👇�👇�👇�
*_1 Wakorintho 15 : 34 - Tumieni akili kama ipasavyo, wala msitende dhambi; kwa maana wengine hawamjui Mungu. Ninanena hayo niwafedheheshe._*
✍�Unashauriwa kutumia akili ipasavyo, sasa waweza nusuru ndoa yako, mahusiano yako kwa kutumia akili hii hapa.
❤❤ *RADHA YA NDOA*❤❤
_Mwana ndoa Radha yote ya ndoa ipo hapa, siyo kwenye magari yako, pesa zako, PhD zako wala uzuri wako, kazania hapa_
✍� *_Baba mke wako anahitaji kusikia kila mara neno NAKUPENDA MKE WANGU,_* Hii ni miongoni mwa dawa ya hatari kwa ndoa maana ukishasema nakupenda mke wangu, haipo siku utawaza kumsaliti, hauta mpiga, hauta mtukana, ila utampenda, utamtunza na kumjali. (Asipo sikia neno hilo, furaha yake inapotea, na ikipotea ndo mwanzo wa migogoro ya ndoa)
✍� *_Mama mmeo anahitaji kuona unaangaika kumtimizia haja yake_* mmeo anataka kuona ametoka kazini, au safari unaangaikaje kumuhudumia,? Apate maji ya kuoga, chai/juice, chakula umeandaa kitanda apumzike nk.
✍� *_Baba, mkeo anahitaji kusikia ukimsifia, wewe mzuri, umependeza leo nguo yako, ulivyo suka nk_* mara nyingi mambo mengi wanawake wanafanya ni kwaajili yako mme wake, akivaa, akijilemba, akisuka anategemea kuna Neno litatoka kwa Mr, kwamba nimependeza. (Akilikosa sasa atachomoka nawale wanao msifia, moyo utahama kwako, ataanza kutamani kuzurura ili watu wageuke, wapige miruzi, wamsifie ndo anaridhika) *_Wanaume hawa watu Wanapendaga sifa_* usipo mpa sifa anakudharau moyoni na anaona hukidhi viwango vya kuitwa mme, maana waume wengine nje wana sifia balaa.
✍� *_Mama mmeo anahitaji kuona lugha yako niya upole, na unamsikiliza_* mwanaume ameumbwa kuwa mtawala, ukitaka Amani, msikilize, mshauri kwa upole, ndani ata akikosea usipayuke na kukoroma kama unamkoromea mwanao, mwambie, *_Lakini mpenzi wangu hapa umenikwaza, sijajisikia vizuri_* inatosha, kwani ukivimba na kuzira ndo utambadirisha, huyo anaitwa kichwa, mme, mtawala, kuwa mpole tu utaona ndoa itakavyo noga.
✍� *_Baba, mama mwenzako anahitaji kusikia unamuita jina zuuri analo lipenda_* Radha kubwa kwa mpenzi wako, katafute kote duniani, kama (Mchepuko/Hawala) anamwitaga mmeo, mkeo... Mama John, baba Joyce, au anamuita... Peter, Makulata📢📢) haipogo hiyo, wanaitana ( *_Honey, Baby, Mpenzi, Sweet, Love nk_*) Ndo maana mnaibiwa waume na wake zenu, jina zuri lina nguvu kubwa kwa mtu (ndo maana Biblia ikasema Heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi *Mithali 22:1*) sasa endelea kumuita mwenzako Makulata, wenzako wanamuita Honey, au muite baba Kristopher wenzako wanamuita Hubby wangu. Ndoa hiyo umeiuza.
✍� *_Baba, mama mwenzako anahitaji kuona pale tu anapo kuambia tucheze mchezo wetu, unafurahi na kumwambia haina shida mpenzi wangu hilo tu? Twende nikupe raha_* Fatilia makahaba wote wanaoinmba waume za watu na wake za watu kama huwa wana udhuru kwenye tendo la ndoa, walo 🆓 24hrs, sasa wewe mpaka udanganywe, utegeshewe kama panya na karanga ndo aingie mtegoni! Hujui kulinda ndoa. _Mwenzako akikunong'onezea uhitaji onyesha support kubwa, na asione kama umelazimishwa, na kama hauko vizuri tumia ufundi mkuu wa kumshawishi kwa amani muahirishe mchezo mtoe pointi 3 za mezani._
✍� *_Baba, mama mwenzako anahitaji kupata zawadi kutoka kwako_* Unajua zawadi si lazima iwe kubwa, zawadi ni Ishara, au kiwakilishi cha hisia zako juu ya mwenzako kwamba una mpenda, unamjali, unamthamini, ni special. Kwa hiyo jifunze kumtafutia zawadi mwenzako hata chocolate, pipi ukiileta rasmi kwaajili yake ni kubwa kuliko kumpa pesa laki moja ya matumizi huku na masimango.
💈💈 _Kwa leo niishie hapi, anza na hayo, siku nyingine ntakuletea mengine, ulikuwa nami Mchambuzi Mtaalamu wa Mahusiano na Ndoa, Ev. Elisha Kazimoto(Baba Eve), kwa masomo zaidi Tembelea Facebook kwa jina la Elisha Kazimoto, utakutana na Pages 3 za nafundisho yangu, Like, share utakuwa umejiunga nami. Na kwa ukaribu sana, mada, maswali na majibu njoo Whatsapp kwa no. 0755444078, uombe kujiunga na chuo mafundisho kiitwacho *MATERIAL ADIMU UNIVERSITY 🎓* kama utafaulu Interview. Ni mafundisho Chini ya Maadili ya Kiroho (Mahusiano, Uchumba na Ndoa)_💈💈
*By Ev. Elisha Kazimoto*
*0755444078*
No comments:
Post a Comment