🛜🛜 *UKIZEMBEA YATAINUKA MAWE KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKO* 🛜🛜
_Hili ni Neno la Kibiblia ila linanipeleka mbali mpaka kuyazumgumzia Mahusiano ya wana ndoa wa Kizazi cha Sasa_
*40 Akajibu, akasema, Nawaambia ninyi, wakinyamaza hawa, mawe yatapiga kelele.Luka 19:40*
🛜We msomaji wangu anzia msitari wa 37, upate kisa kamili, sasa mimi mchambuzi kwakuwa sihubiri neno hapa, ila nachambua kisaikolojia ndoa kwa msingi wa Sentensi ya Kisaikolojia ya Luka 19:40, *_Hawa wakinyamaza Mawe yatapiga kelele_* Nisikilize vizuri nikusaidie kitu hapa.
🛜Katika Mahusiano (hasa ya ndoa) Kila mtu ana WAJIBU na Majukumu yake ya kutimiza ili kuimarisha Furaha na Upendo kwa wana ndoa hao.
🛜Kinachotesa na kusumbua ndoa nyingi pamoja na hila za shetani, ila ni Mwanandoa Mmoja wapo au wote *Kusahau, Kupuuzia, Kuacha Baadhi ya Majukumu muhimu yanayo muhusu kwaajili ya mwenza wake*
🛜Katika Msitari huo 37-40 unaona kuna Watu walitakiwa na ilikuwa ni wajibu kuna mtu inabidi wa Mwimbie, Wamtukuze, Wamsifu, Washangilie,wapige kelele kwaajili yake, Lakini kuna kundi la watu Wakawa wana mawazo ya Kuzuia kelele zile na sifa zile.
🛜Hawakujua umuhimu wa zile sifa na kelele anazopewa yule mtu(Yesu) au walijua ila WIVU TU, ndo uliwatuma.
🛜Sasa wao wakadhani kwakiamuru watoa sifa na kelele KUNYAMAZA watakuwa wamemkomoa Bwana Yesu.
🛜Yesu akataka kuwambia ukweli, kwamba *Sifa, Heshima, Kelele na Utukufu ni LAZIMA siyo muhimu tu* nilazima nipewe, ndo maana NINYI MKIKATAA NA MKAZUIA HAWA wasinipe NINACHO STAHILI, *Mawe Yatainuliwa Yafanye kazi ile ile iliyobidi ifanywe na hawa*
🛜Wana ndoa mnapo poa mnaanza kuruhusu MICHEPUKO?(Mawe hayo) yanainuka kufanya kazi ile ile, *_Ya Kutoa Matumizi, Kusifia, Kuongea naye kwa Mahaba, Kumpa Penzi kwa style zote na mbwembwe zote na furaha yote na muda wowote ANAPO LIHITAJI PENZI_*
🛜Kazi iliyokuwa ya wanadamu( mwanandoa) Inashikwa na Jiwe(Mchepuko).
🛜Unapaswa kujua jiwe halina mamsikio, wala alioni, na halina huruma likisha pewa kazi linafanya kazi mpaka litakapo pasuka au tupwa.( Ndo maana ndoa nyingi zinaugulia maumivu ya muda mrefu) jiwe haliachii karibuni.
🛜 Mwana ndoa, Unajua *_Mmeo/Mkeo Kipi kina mtesa kwako? Anachokihitaji sana, anachodai sana,kinachomfurahisha sana_* Aisee kuwa makini kifanye kwa gharama zozote Ukidharau ukahisi Unamkomoa, My friend Yakiinuka Mawe Kuanza Kupiga Kelele Uwezi Nyamazisha! Itakuwa imekula Kwako.
_Mwisho, kila mmoja kwenye mahusiano kuna kitu kina msumbua sana anakihitaji kwa mwenzake sana, wengine Heshima, wengine Pesa, wengine Kusikilizwa, Wengine kuhurumiwa, Wengine Kupendezeshwa, Wengine TENDO LA NDOA, wengine Kufanya Maendeleo, haya yote kila Mmoja anatakiwa Akae mkao wa Kuwajibika, Ukidharau na Kuona kawaida, Anayekihitaji Aoni kawaida, Atakacho Fanya Atatafuta Mawe ya Kupiga kelele maana tayari wanadamu Wamenyamazishwa, anatafuta kisicho nyamazishwa, na jiwe likianza kupiga kelele uwa linapiga kelele bila kuchoka likijua lenyewe halina sifa ya kupiga kelele limeokotwa tu kama mbadala, ndo maana halichoki, haliangalii changamoto lenyewe linajua likicheza Binadamu anarudi kwenye nafasi yake ya sifa. Tuzuie Mawe Kupata nafasi ya Kupiga Kelele kwa Kila mmoja kumtimizia Furaha Mwenza Wake_
*Ulikuwa nami Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa Ev Elisha Kazimoto(CEO-GFI) 0755444078*