🎁2️⃣0️⃣2️⃣1⃣ *MWAKA WA KUACHILIWA(MWAKA WA MAACHILIO)* 2️⃣0️⃣2️⃣1⃣🎁
_Mnenaji Ev Elisha Kazimoto(0755444078)_
_Shalom watu wa Mungu mliopata neema ya Mungu Kuingia katika mwaka mpya wa 2021,Heri ya Mwaka Mpya kwako unaye soma Ujumbe huu na *Neno la Kinabii* la mwaka huu. Kila mwaka Bwana amekuwa akinipa neno la Mwaka mzima,na katika mwaka huu hili ndilo Bwana ameninong'oneza katika usiku wa tarehe 31.12.2020 katika mkesha wa Mwaka mpya,tukiwa katika maombi ya kumshukuru Bwana na kuukaribisha mwaka mpya 2021, *Nikanong'onezwa na Roho wa Bwana akisema, Huu mwaka mnaouingia ni mwaka wa Kuachiliwa(Maachilio)* tangu muda huo maombi yangu yalibadirika nikaanza kuunena mwaka tunaouingia niwa Kuachiliwa kwa vitu vingi Vilivyo shikiliwa muda mrefu, sasa nikukaribishe katika ujumbe huu kama unaamini Neno la Bwana utashuhudia mwenyewe kabla ya mwaka huu kuisha mambo mangapi yako yaliyokuwa yamezuiliwa sasa YAMEACHILIWA_
*_1 Bwana akamwambia Musa, Liko pigo moja bado, nitakaloleta juu ya Farao na juu ya Misri; baadaye atawapa ninyi ruhusa mtoke huku; naye hapo atakapowapa ruhusa, atawafukuza mtoke huku kabisa kabisa.Kutoka 11:1_*
🌲Watu wengi muda umepita,miaka imepita hawaoni wanayoyaomba,pamoja na kwamba wakijichunguza wanaona wako vizuri na Mungu,siyo hivyo tu ila kama kuomba na kuombewa wameomba na kuombewa ila *Mambo hayatokei,bado yamezuiliwa*
🌲Ndivyo ilivyokuwa hata kwa wana wa Israeli,miaka mingi wako chini ya mateso,mkombozi amekuja (Musa) ameanza harakati za kuomba(maombi) kibali cha kutoka,siyo kwa hisia zake no kwa maelekezo ya Mungu, fanya hivi mtatoka(MTAACHILIWA) Lakini wapi(tangu sura ya 3 ya kutoka Mungu anakiri kuona kilio chao na kusema sasa nimeshuka kuwaokoa,mpaka sura ya 11 Mungu anasema sasa Liko pigo 1 nikilileta huyu aliye wang'ang'ania ATAWAACHILIA KABISA KABISA,haikuwa kazi ndogo na muda ulikuwa umesonga.
👉Nataka niseme nawe unayesoma ujumbe huu wa Kinabii, 2020 nakurudi nyuma ulitembelea ndani ya kipindi cha ( *Sura ya 3 hadi 10 ya Kitabu cha kutoka*) mwaka huu ulipoanza(2021) UMEINGIA SURA YA 11 SURA YA MAACHILIO.
🌲Mungu anamwambia Musa pigo hili litamfanya Farao AWAACHILIE nanyi mtatoka huku KABISA KABISA.
👉Kuna sehemu utatoka kabisa kabisa mwaka huu, *_Mwaka huu unatoka katika masimango ya wanadamu,unatoka katika magonjwa,unatoka katika utasa,unatoka katika kutooa au kuolewa,unatoka katika dimbwi la madeni na umaskini, Vitu vyako vinaachiliwa katika jina la Yesu_*
👉👆 _Mme wako anaachiliwa kutoka kwa makahaba,mtoto wako anaachiliwa,elimu yako inaachiliwa,ofisi yako inaachiliwa,ndoa yako inaachiliwa,mume wako,mke wako,mahusiano yako YANAACHILIWA KATIKA JINA LA YESU_
🌲Sijui kama unaelewa na unaona ninachokiona,kama kukata tamaa ilibidi Musa akate tamaa haraka, maana alikuwa anaambiwa na Mungu fanya Ishara hii Farao atawaachia, anafanya na FARAO HAWAACHII,anarudi kwa Mungu mbona amegoma kutuachia?Mungu anampa ishara na pigo lingine anafanya,Farao anagoma kuwaachilia Israeli watoke kwenye mateso, ila sura ya 11 Mungu anasema LIMESALIA PIGO 1 HILO NI LA MAACHILIO, wacha *Mungu mwaka huu ampige adui yako pigo moja la mwisho,PIGO LA MAACHILIO naye ATAKE ASITAKE ATAACHILIA mipango yako na maono yako na huduma yako*
🌲Kwanini una mashaka? Kwakuwa umeomba sana na kuombewa,?umetabiriwa sana hujaona? Wewe ungekuwa Musa ungewatoa Israeli kweli Misri? Aaah Huu ndo Muda wa Mungu unaposoma ujumbe huu SAA YA KUACHILIWA IMEFIKA...Anza maandalizi ya kutoka,weka mipango yako sawa,andika maono yako ya mwaka mzima sasa,fanya ulilolikusudia 2021 ni mwaka wa *Kuachiliwa kwa vitu vilivyo shikiliwa*
🎁 _16 Ndipo wale waliomcha Bwana waliposemezana wao kwa wao. Naye Bwana akasikiliza, akasikia; na kitabu cha ukumbusho kikaandikwa mbele zake, kwa ajili ya hao waliomcha Bwana, na kulitafakari jina lake. Malaki 3:16_
*_17 Nao watakuwa wangu, asema Bwana wa majeshi, katika siku ile niifanyayo; naam, watakuwa hazina yangu hasa; nami nitawaachilia, kama vile mtu amwachiliavyo mwanawe mwenyewe amtumikiaye.Malaki 3:17_*
👉Mungu yuko kazini mwaka huu kushugulikia watu wake na mambo yao ambayo yalikuwa yameshikiliwa muda mrefu sasa anasema Ataachilia. Hakuna adui wa kuendelea kukuchezea akishikilia vitu vyako,kazi yako ni *Kukaa na Mungu sawa sawa na kumwamini na neno lake* Mwaka wa Maachilio.
🎁 _20 Basi Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni kinyume cha hirizi zenu, ambazo kwa hizo mnaziwinda roho za watu kama ndege, nami nitazitoa katika mikono yenu kwa nguvu; nami nitaziachilia roho zile mnazoziwinda kama ndege.Ezekieli 13:20_
_21 Na leso zenu nazo nitazirarua, na kuwaokoa watu wangu katika mikono yenu, wala hawatakuwa katika mikono yenu tena kuwindwa; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana.Ezekieli 13:21_
👉👆Kwa namna yoyote waliyokuwa wamekushikilia adui zako,iwe kwa uganga,mahirizi,walikufunga leo usione uendako na usionekane, Mwaka huu Bwana anasema ATAZIRARUA LESO HIZO walizokufunga ili Akuachilie wewe.
_Nimalize kwa kusema hivi, Suala la Kuona kile Mungu alichosema na watumishi wake kwa unabii,haliko mikononi mwa Mungu,bali mikononiwa Asikiaye neno la Mungu,ukiliamini na kulifuata UTAONA,ukidharau na kutoamaini HUTAONA BADILIKO LOLOTE ila waliomgoja Bwana Muda mrefu na wamesikia na wanaamini sasa NATANGAZA KATIKA JINA LA YESU KITU CHAKO KILICHOSHIKILIWA KWA MUDA SASA KUACHILIWA MWAKA HUU 2021 Hilo ndilo neno la Bwana,mwenye kulipokea na kuliamini Pokea nguvu ya Maachilio katika jina la Yesu Amen_
🎁Ulikuwa nami mnenaji wako, Mtumishi wa Bwana na mjumbe wa matengenezo wa nyakati za mwisho, *Ev Elisha Kazimoto(Whatsapp 0755444078)*
Facebook Ev Elisha Kazimoto.
©️2️⃣0️⃣2️⃣1⃣