💎💎 *PESA (MSHAHARA KATIKA NDOA) NI SUMU NA NI UPONYAJI*💎💎
_Anachambua mwanasaikolojia na Mshauri na Mtumishi wa Mungu *Ev Elisha Kazimoto* fuatana naye ujiongezee ulinzi wa ndoa yako_
................
................
*MFUMO WA KIUCHUMI KATIKA NDOA UNAOWEZA KULETA AMANI YA NDOA NA MAENDELEO YA FAMILIA*
_Uchumi(pesa )katika familia kwa wana ndoa imekuwa changamotl ya wengi,kiasi kwamba watu wanaishi kana kwamba ni *Watu waliokutana forb Part time* siyo wanandoa,na kana kwamba ni washirika wa muda katika ndoa na si wana ndoa wa kudumu_
👉Hii changamoto imekuwa kubwa sana hasa *Kwa Wafanyakazi na wafanya biashara ambao wote mke na mme wana kipato binafsi* hawa ndo wana maisha mabaya ya kindoa na kiroho.
👉Pesa kwa wana ndoa imekuwa Sumu ya kuwagawa na kuwafanya wawe watu wawili ndani ya mmoja.
👉Shida kubwa hapa Siyo Pesa, *Shida ni Akili ya Kindoa* ndiyo imekosekana.
👉Kuna watu wanaingia kwenye ndoa wakiwa :
🏹Hawajakomaa kisaikolojia na Kiakili kwaajili ya ndoa(kuna kukomaa kiumri ila usikomae kiakili)
🏹Wanaingia kwenye ndoa bila kujua *Falsafa ya Mungu kuhusu ndoa*(Si wawili tena bali mwili mmoja), hiyo ya kwanza......Kwa hiyo watu wanaingia kwenye ndoa *Anaendelea kujiona yeye mwenyewe baada ya kumuona mwenzake* kwa hiyo wanaishi Kama watu wawili tofauti wenye agano la kuwa mmoja.
🏹Falsafa ya pili, Mungu amesema *Mtu ataacha baba yake na mama yake,naye ataambatana na mmewe*(Wengi wakiingia kwenye ndoa Hawaachi wazazi wao au ndugu zao kisaikolojia,kimwili wanakuja nao)ndiyo maana wanaendeleza ubinafsi wa kuwaza juu ya familia yake yeye kama yeye na si wawaze pamoja (mke na mme)juu ya familia zao.
🏹 *Sasa nisikilize kidogo hapa shida ya wana ndoa wenye vipato wote kwa nini ndoa zao ni changamoto, zaidi ya ndoa za maskini au za mtu mmoja mwenye kipato....*
1⃣Ukishindwa kujua *Ukishaoa au olewa unaanzisha Taasisi mpya* inayokuhusu wewe na mwenzako TU( ikiwa nzuri ni heshima kwako,na ikiwa mbaya ni dharau kwako) jua ya kwamba Utakuwa miongoni mwa walioolewa au oa bila kukomaa Akili na lazima ndoa yako italeta shida.
🏹Kwa hiyo basi Kama umeoa na kuolewa jua ya kwamba *KIPATO CHAKO, LENGO LA KWANZA NI KUJENGA TAASISI YAKO MPYA NDOA* wengine wazazi,ndugu, kazi ya Mungu vinafuata hapo.(Ukikosea hapo ukahisi KIPATO CHAKO ni kwaajili ya kusaidia wazazi,ndugu,na kujipamba,jua wewe ni Miongoni mwa watu ambao ulikuwa bado mchanga kuingia kwenye ndoa,au Hukujaliwa akili ya Kimaisha na uwezi kuwa na future ya maendeleo na baraka za Mungu)
*Note:Ukioa au Ukiolewa, kipato chako ni kwaajili ya Kujenga Heshima ya Taasisi mpya uliyoiingia* na Taasisi ya ndoa Haijengwi na mtu mmoja,inajengwa na wawili,mmoja akijichomoa na kuona mmoja(mme au mke)ndo atumie kipato chake kujenga Taasisi ya ndoa,jua *Ulioa au uliolewa na Mlemavu wa Akili* asiyeweza ku make future nawe, kwa hiyo suluhisho siyo kumwacha, ni kwenda na mzigo huo mpaka Mungu akusaidie au atakapofundishika,au Uamue kumfundisha kwa vitendo.(hilo ni somo lingine)
2⃣ *Ukishindwa kujua kuwa kwenye ndoa ( Ya watu wenye Akili) vipato na vitu vyote ni vya kwenu siyo vyako(uwe ni mshahara au biashara) jua kuwa Wewe bado ulifaa kuishi peke yako au na ndugu zako siyo mme au mke*
🏹Kuna maajabu ya wana ndoa kila mtu na mshahara wake,na matumizi yake,kiasi kwamba hakuna anaye ruhusiwa kuingilia kioato cha mwenzake, hata mmoja akiishiwa *Ataomba kukopeshwa na Mwenzake*(wana ndoa hao) Hii ni ndoa ambayo ni marehemu anaye tembea,lakini hawawezi kuenjoy maisha ya Raha ya ndoa,wataishi kwasababu wanaweza kuishi kwa nguvu ya pesa siyo nguvu ya Mahaba.
🏹 Wana ndoa yenye wafanyakazi wawili wenye vipato au wafanya biashara wote wana kipato, wanafursa ya kufanya mambo makubwa kwa mafanikio na amani zaidi.
🤝 *Kuwa wazi kwa kipato chako kwa mwenzako,muwe na asilimia mlizokubaliana za jumuisho la pesa za kufanya mambo ya familia,na asilimia zingine mtu anaweza fanyia private issues au kwa kumsurprise mwenzake*
🏹Ni upagani na utoto wa akili, kuficha kipato chako kwa mwenzako kwa kisingizio cha *Kipato chako ni cha mambo yako mwenyewe na familia yako* wewe hukufaa kuoa au kuolewa, (NDOA NI COMMUNAL OWNERSHIP SIYO CAPITALIST SYSTEM (PRIVATE OWNERSHIP )
🏹Kinachoondoa amani kwa ndoa nyingi ni UMIMI KATIKA UCHUMI, suala la kusaidia wazazi na ndugu zenu ni suala la mipango ya pamoja kuangalia kipato chenu kwa ujumla na ni kiasi gani mwaweza tenga kusaidia familia zenu.
*NB: Wadada mnaofanya kazi na biashara hamjaolewa kuweni makini sana na dhana ya mme ndo anawajibu kutunza familia,na kipato chako ni kwaajili ya kujiremba na wazazi wako na ndugu zako,huo ni utoto na ushetani wa kuipundua kanuni ya Mungu ya kuwa kitu kimoja na kushindwa kuleta maendeleo*
🏹Lakini wavulana kabla ya kuoa au kuolewa *Dadisi sana kujua mtazamo wa mchumba wako kuhusu matumizi ya kipato chake,ukihisi dalili za ubinafsi wa kipato Huyo siye mke ni Mshirika wa mapenzi PIGA CHINI,bora uoe mpika vitumbua na chapati*
🏹Kuna mabinti uwa wana lugha ya Unaoa mimi *Huoi mshahara wangu* mshahara wangu utatunza wazazi walionisomesha, Hawa mara nyingi uwa wanachelewaga kuolewa kisaikolojia na Kimungu,uangukia mikononi mwa wanaume jeuri kimakusudi,ili wanyooshwe.
🏹Ni hakika mwanaume ndiye Anawajibu wa Kuhakikisha familia inasonga, je wewe mwanamke kama mratibu mkuu na msaidizi wa mfumo mpya kazi yako nini? Ni kuhakikisha mmeo Halemewi lakini unaweka mazingira ya kuchochea Maendeleo na mafanikio ya familia yenu.(Kumbuka nanyi mtazeeka,mtakuwa na watoto na wajukuu) mnavyochelewa kuunganisha nguvu pamoja ili mkimbie kimafanikio,ndivyo mtakavyo lemewa kubeba familia.
*MWISHO OA AU OLEWA NA MTU MWENYE AKILI JUMUISHI SI AKILI BINAFSI NDO MTATOBOA KIUCHUMI,KIROHO NA KISAIKOLOJIA*
By Ev Elisha Kazimoto(Psychologist and Counselor )