🫂🫂 *SWALI KWAKO MWANA SAIKOLOJIA NA MTUMISHI WA MUNGU EV: ELISHA KAZIMOTO* 🫂🫂
_"Kumekuwa na Malalamiko na Manunguniko kwa baadhi ya wanandoa Hawako Huru na Miili ya wenzi wao iwe mchana au usiku na hasa Utamaduni wa kulala na Nguo kwa Mwanandoa,iwe moja ya ndani au full hii imekaaje?_
..........................................
*_Nitajibu kamaulivyoniuliza, ila majibu yangu yatakuwa marefu kidogo Nitoe Elimu, Darasa la Kisaikolojia Katika Ndoa kwa wana ndoa,kuliko ya kujibu kwa ufupi kwamba si sawa au ni sawa, Nitoe ufafanuzi wa kina kama part 2 mpaka 3 au 4 Jitajidi usome zote, Kufikia Mwisho Usipo Pata Kuelewa na Kubadirika kama Mwana ndoa Jua Wewe Hukutakiwa Kuolewa au Kuoa ilibidi Ufe ukiwa Single_*
Uko Nami Mchambuzi wa Masuala ya Ndoa na Mahusiano Ev Elisha Kazimoto( 0755444078)
...........................................
💚💚💚💚💚💚💚💚💚💚💚
👉Wana ndoa tunahitaji kujua kitu kinaitwa *PSYCHOLOGICAL ETHICS OF MARRIAGE* (Tafsiri isiyo Rasimi.... Saikolijia ya Maadili ya Ndoa)
Kwani unadhani ndoa ni ngumu? Nooo Tuna kwama kwenye Maadili ya Ndoa ya kisiakolojia yake.
👉Leo nitoe darasa kidogo kati ya maandiko yangu nimeandika juu ya ndoa(ukienda kwenye blog yangu au Google andika *Material Adimu University* )utakuta maarifa mengi yatakusaidia kwenye mahusiano na ndoa hata Huduma yako.
1️⃣Wana ndoa, Saikolojia inasema Ndoa ni *Uwanja Huru na wa Uchaguzi kwaajili ya Kujipa furaha ya Mwili, na Akili*
👉Hapa kuna vitu vingi tunavikosea sana wana ndoa, na Kwa hali hiyo *Usaliti, Uchepukaji, na Uzuri wa Mmwenzako Kupungua machoni pako na akili mwako havitaisha* mpaka pale wana ndoa tutaacha Ubabe na Ujuaji na Misimamo binafsi inayoua HISIA ZETU.
👉Wana saikolojia wanapokwambia ndoa ni Uwanja Huru...Wana maanisha, *Jitahidi sana Umfanye mwenzako Ajisikie Uhuru kwako kuanzia mwilini Mwako ajisikie yuko huru na mwili wako, Ajisikie huru kukupa mawazo, ajisikie huru kukukosoa, ajisikie huru kuku brand kwa marafiko zake au kwa watu, ajisikie huru kujieleza shida,changamoto na uhitaji wake*
👉Ukiona Una mnyima Mwenzako uhuru wa Baadhi ya vitu ambavyo Hakika anajua Ni Haki yake Kuwa huru navyo *Basi saikolojia inasema Atavipata tu kwa njia yoyote na popote bila kujalisha ni salama au si salama,ni wazi au siyo wazi*
👉Kosa si lake, kosa ni la Aliye mnyima uhuru,. Japo kama ni kosa kiufundi ni la mtenda siyo msababishaji ila wanasaikolojia tunaamini Kosa limesukumwa na mtu.
NB: *Hapo Umejifunza nini kama mwana ndoa kwa point ya kwanza?*
👉Wanasaikolojia wanapo sema Ndoa ni Uwanja wa Uchaguzi,.... *Wanamaanisha Alipo kuchagua kuwa mme au mke wake alijua hakika Wewe Utampa Furaha*
👉Pili katika kile Kikubwa alichokichagua, kila siku na kila saa ana machaguo yakeadogo madogo ya *Nini kitampa furaha kwa wakati mfupi mbali na wewe kuwa furaha yake ya kudumu maisha yote*
👉Anaweza CHAGUA SEX impe furaha muda huo( Je wewe upo tayari?),Anaweza akachagua Kupiga story nawe za Mahaba, je wewe huko tayari?, Anaweza akachagua Kukupa Zawadi au Anategemea Zawadi kwa kipindi flani,je wewe uko tayari? Anaweza kuchagua kutaka kusifiwa au kupongezwa,je wewe huko tayari? Anaweza kuchagua Mcheze michezo ya kimahaba,mapenzi,je wewe huko tayari!
👉Utafiti wa Kisaikolojia unaonyesha, Wanandoa wengi walio dumu kwenye ndoa miaka 10 kuendelea *Wamepoteza Utayari kwa wenzi wao pale wenzi wao wanapo Kuwa na Machaguo ya kuwapa furaha*
👉Ndiyo Maana wengi wameshangaa waume zao au wake zao waliokuwa Waaminifu kwao ila sasa Wameanza Kuwa Cheat! Si kwamba Udanganyifu kwenye ndoa umetokea kama TABIA YAKE NOOO NI MAZINGIRA yaliyo tengenezwa na mwenzi wake kwa Kukosa Utayari kwa Machaguo anayo yachagua mwenzi wake.
👉Saikolojia inasema, *Kila chaguo lililo chaguliwa na mtu, ila mwenza akakosa utayari Litatafutiwa Mbadala wa Utayari kwa mtu mwmingine ili Gap la kisaikolojia la furaha Lizibwe*
NB: Gap likizibwa na mtu mwingine asiye sehemu ya ndoa linaweza kuwa chanzo cha kumpoteza mwenza jumla.
👉Saikolojia inapozungumzia *Furaha ya Mwili* aaah hapa aisee wana ndoa Turudi darasani na Tutulie kweli, Hapa kwa waliookoka msikemee mapepo kwenye ndoa ukiona mabadiriko kwa mwenza wako,Tulia ujihoji halafu kimya kimya anza mchakato wa mabadiriko mbali na hapo, Kuna maisha magumu unayaandaa mwenyewe bila kujua kumbe ungelijipa raha duniani na maisha yenyewe haya mafupi.
💚Kila mwana ndoa au niseme Binadamu anahitaji Furaha ya Mwili, sasa mimi hapa niko kwa wenye ndoa zao, wana saikolojia wanaposema, mtu anatafuta Furaha ya Mwili kwako elewa mambo haya:
🤝Kuna mtu anahisi raha kama akikukumbatia mkiwa mmelala(mwili wake anahisi raha)
🤝Kuna mtu anahisi raha iliyoje kama Aki Romance na wewe wakati na nje ya tendo la ndoa(mwili wake unatulia)
🤝Kuna mtu anajihisi raha akichezea Maziwa yako,kifua chako, hips zako, garden zako Ukiwa necked( anapata furaha sana)
🤝Kuna mtu anajihisi Raha akiwa kitandani nawe *Ukiwa Free mwilini mwako Hakuna Nguo Yoyote* ile ngozi kwa ngozi zikigusana (Ahaaa anahisi raha) yaani hapo ni nje ya tendo la ndoa.
🤝Kuna mtu anahisi raha ya mwili wake pale anapo shiriki tendo la ndoa nawe (Anahisi raha ya ajabu).
NB: *Sasa hatari ni nini? Ni pale mtu ametegemea furaha ya mwili wake aipate kwako na wewe Ukazuia, Jua moja kwa moja Furaha ya Mwili Itatafutwa tu Pengine.*
👉Sailolojia haijawahi kukaa na SHIMO WAZI (gap) mpaka lizibwe sasa hapo ndo kuna hatari ya ndoa na familia.
👉Wana saikolojia wanaposema..... *Furaha ya Akili* hapa napo pana tesa wengi, hapa kuna watu wana misongo ya mawazo, uchumi mgumu, taarifa mbaya, na masumbufu mengi ya maisha, sasa Eneo ambalo uwa lina ponya na kuwapa watu matumaini kama alivyokuwa ameumba Mungu ni Ndoa(Mwenza wako)
👉Kuna vitu ukifanyiwa vina leta furaha kwenye Akili yako na Unasahau changamoto kwa muda, siku na muda unakuwa unasogea.
1.Romantic Chatting ( mtumiane sms za kimahaba na za upendo na amani)
2.Sex play mcheze na kutaniana kama wachumba au kama wapenzi wapya.
3.Muitane majina ya kimahaba.
4.Mpongeze au msifie kwa kila kazi atakayo fanya au jambo atafanya.
5.Angalia Anatoa Ishara ya Kutaka sex,mwitikie positive bila vijisababu vya kuahirisha.
👉Haya mambo 5 yanaleta furaha ya Akili, Wewe Usipo mpa mambo haya 5, Atatafuta Eneo lolote la Kuyapata ili Akili Ituliepo, Aaipo Pata pa kutuliza akili ndo mtamuona mtu anadalili hizi.
1.Mahasira ya mara kwa mara.
2.Majibu ya mkato/ kukaa kimya
3.Anakaa mtandaoni sana kuliko na wewe.
4.Hafanyi jambo lolote kwako au kwenye familia yake mpaka mmemdai kitu flani.
NB: *Tuokoe familia zetu na ndoa zetu kwa Kurudi kwenye Maadili na Saikolojia ya Ndoa*
_Imeandaliwa na Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa, Mwana Saikolojia *Ev Elisha Kazimoto*(C.E.O- wa G.F.I)
Whatsapp 0755444078
E-mail : babaeve755@gmail.com